Pages

Saturday, December 7, 2013

HAWA NDIO VIONGOZI WAKUBWA DUNIANI AMBAO WATAKUWEPO KWENYE MAZISHI YA MZEE MANDELA

Afrika Kusini leo imeanza maandalizi ya kupokea ugeni mkubwa wa viongozi wa dunia akiwemo Rais Barack Obama wa Marekani wanaoenda kutoa heshima zao za mwisho kwa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma jana alitangaza siku 10 za maombolezo kufuatia kifo cha kiongozi huyo wa zamani  anayependwa zaidi duniani. Obama, ataenda Afrika Kusini wiki ijayo na ataambatana na mke wake  Michelle pamoja na Rais wa zamani George W. Bush na mkewe Laura Bush.
Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, ambaye alikuwa madarakani wakati Mandela alichaguliwa kuwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini naye amesema ataenda na familia yake. Mwili wa Mandela utalazwa mjini Pretoria kwa siku 3 kabla ya mazishi yatakayofanyika December 15 katika kijiji Qunu alikozaliwa.
Kufuatia ugeni huo wakala wa usafiri wamesema kutakuwa na malazi nadra katika miji ya Johannesburg na Pretoria na tayari serikali ya Afrika Kusini imeanza kuzuia booking za vyumba kwenye hoteli.
Wakati huo huo wataalam wa masuala ya uchumi wamezitupilia mbali hofu za kuwa kifo Nelson Mandela kinaweza kusababisha madhara ya kiuchumi na kifedha kwa Afrika Kusini.
Wachambuzi wamesema soko la hisa la Johannesburg jana Ijumaa limeendelea kuwa imara tofauti na watu wengi waliodai kuwa kifo cha Mandela aliyekuwa na umri wa miaka 95 kingeweza kusababisha anguko la uchumi.

0 maoni:

Post a Comment

Matangazo

Matangazo

Popular Posts

 

Blogger news

Blogroll

About