Pages

Friday, November 8, 2013

Upendo wa Papa Francis washangaza ...cheki alichomfanyia huyu aliyetengwa!

Picha mpya zinazomuonesha papa wa kanisa katoliki Pope Francis akifanya kazi ya kumbariki na kumfariji mtu ambaye si msafi zimesambaa kwenye mitandao duniani.

Pope Francis alikuwa kwenye wiki yake ya kuhutubia hadharani ambapo alijitokeza mwanaume aliyekuwa na matatizo ya kuvimba mwili na kuomba baraka za Papa.


Mwanaume huyo anakabiliwa na ugonjwa unaomsababishia maumivu makali na kutokea uvimbe wa mfano wa vipele vikubwa ugonjwa ambao kitaalamu unafahamika kama neurofibromatosis, wakati mwingine ukitajwa ni kama aina Fulani ya kansa ya ngozi,ugonjwa ambao pia umekuwa ukimsababishia kutengwa na jamii kwa kuonekana sio msafi.

Watu wakashangazwa na Pope Francis ambaye alimbusu usoni na kumbariki kwa ishara ya msalaba huku pia akionekana kuzama kwenye maombi ya kumuombea mwanaume huyo.

Fuatilia picha ya tukio hilo.
 
 
 
 

0 maoni:

Post a Comment

Matangazo

Matangazo

Popular Posts

 

Blogger news

Blogroll

About