Pages

Friday, November 1, 2013

SAMAHANI KWA PICHA HIZI:ANAYEDAIWA KINARA WIZI WA ‘POWER WINDOW’ AKAMATWA,APEWA KICHAPO NUSURA AFE

 

MKAZI mmoja wa Sinza Lion jijini Dar, Link Mbaga (25) Jumanne iliyopita alinaswa maeneo ya Sinza Afrikasana na kuchezea kichapo kutoka kwa watu wenye hasira akidaiwa kutaka kuiba vifaa vya kwenye gari aina ya Toyota Harrier, Ijumaa limeinyaka. 
Shuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini, alisema Mbaga na wenzake wanne wanaodaiwa kuwa ni vinara wanaounda mtandao wa kuiba power window kwenye magari walifika eneo la tukio wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Noah.
Mbaga akisulubiwa na wananchi.
“Lengo lao lilikuwa ni kuiba kwenye gari la mteja wa Hospitali ya Marie Stop lililokuwa limeegeshwa nje ya hospitali hiyo,” alisema shuhuda huyo.
Gari aina ya Toyota Harrier walilotaka kuiba power window Mbaga na wenzake.
Shuhuda huyo alisema Mbaga na wenzake walifanikiwa kulitoboa gari hilo na kuchukua simu mbili pamoja na kompyuta mpakato ‘laptop’.
“Kabla ya kumalizia zoezi lao mlinzi wa hospitali hiyo aitwaye Jonas Mwakajinga aliwasikia ndipo alipofika na kuwakurupusha,” kimesema chanzo hicho.
Wananchi wakiwa wameandaa tairi tayari kumtia kiberiti Mbaga kabla ya polisi kufika eneo la tukio na kumnusuru.
Inadaiwa watuhumiwa wengine walifanikiwa kutoroka kwa kutumia gari walilofika nalo lakini mlinzi aliwahi kumng’ang’ania Mbaga na kuanguka naye chini.
Wakati mlinzi akipambana na Mbaga wananchi wenye hasira walifika eneo la tukio na walipopata maelezo walianza kumpa kichapo cha kufa mtu mtuhumiwa huyo wakisema itakuwa fundisho kwa wengine.
Kipondo kikiwa kimepamba moto kwa Mbaga.
Wakati akipewa kichapo hicho, Mbaga alijitetea kwamba hakuwa mwizi bali ni mfanyakazi wa kampuni moja ya simu.
“Mimi kazi yangu ni data manager niko maeneo ya Mlimani City, naishi Sinza Lion kwa Massawe,” alisema kijana huyo.


Mbaga akiwa hoi baada ya kichapo.
Mbali na kusema hivyo, Mbaga alidai kwamba ameoa na mkewe anaitwa Fausani na kabla ya kufika hapo alikuwa na rafiki yake wakinywa pombe Mlimani City.
Wananchi wakishuhudia tukio hilo.
“Nilikuwa nakunywa Pombe na Leonard pale Mlimani City, jamani naomba mnionee huruma, wale jamaa walinipa lifti tu,walikuwa wako wanne ila nawafahamu,” alisema Mbaga.

Polisi wakijaribu kuchukua maelezo ya mtuhumiwa baada ya kuwasili eneo la tukio. 

Polisi wakimbeba Mbaga kumpeleka kwenye difenda.
Mbaga aliokolewa na askari waliotokea na kumbeba msobemsobe hadi katika Kituo cha Polisi cha Mwananyamala.
Kutokana na hali mbaya ya mtuhumiwa huyo, askari hao walilazimika kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala ili aweze kupata matibabu.

Mbaga akiingizwa kwenye difenda. 

Safari ya kuelekea Mwananyamala ikaanza.

0 maoni:

Post a Comment

Matangazo

Matangazo

Popular Posts

 

Blogger news

Blogroll

About