Pages

Saturday, November 2, 2013

MWANAMKE AKAMATWA AKIJARIBU KUSAFIRISHA MADAWA YA KWA KUTUMIA MABOGA

Sasa hivi ukisafiri nchi za nje na ukakutana na ukaguza wa kuzidi kiwango cha kawaida katika viwanja vya ndege wala usishangae, sababu biashara haramu ya dawa za kulevya inazidi kushamiri na kusababisha vyombo vya usalama vizidi kuwa makini katika udhibiti.

Hivi karibuni maafisa wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Trudeu huko Montreal, Canada wamemkamata mwanamke mmoja aliyejaribu kupitisha dawa za kulevya aina ya Cocaine zilizofichwa ndani ya maboga matatu.

Maafisa usalama wa uwanja huo wamesema walimtilia mashaka abiria huyo mwanamke aitwaye Mercedes Jerez Farias (26) kutokana na maboga hayo kuwa na uzito zaidi ya ule wa kawaida kwa maboga ya ukubwa huo.

0 maoni:

Post a Comment

Matangazo

Matangazo

Popular Posts

 

Blogger news

Blogroll

About