Pages

Thursday, November 7, 2013

Jay Z anachunguzwa baada ya kumpa zawadi ya gharama mchezaji wa Baseball kwenye birthday yake

Rapper mwenye mafanikio makubwa katika ulimwengu wa muziki Jay Z, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kumpa zawadi ya saa yenye thamani ya $ 34,000, mchezaji wa Baseball Robinson Cano katika siku yake ya kuzaliwa.
Utata huo ulikuja kwa kuwa mchezaji huyo ni mteja anaetumia bidhaa za Roc Nation hivyo kuzitangaza, kwa hiyo zawadi kama hiyo inaweza kuchukuliwa kama hongo ama njia ya kumshawishi mchezaji huyo aendelee kutumia bidhaa hizo.
Zawadi ya Jay Z ilivunja masharti yaliyowekwa na shirikisho la Baseball (MLBPA) ambayo yanakataza kampuni yoyote kumpa zawadi  inayozidi $ 5000 mchezaji wa Baseball anaetumia bidhaa zake,na kwamba endapo itatokea kampuni inataka kumpa zawadi inayozidi kiwango hicho ni lazima iandike barua kwa shirikisho hilo.
Shirikisho hilo limeanza kumchunguza Jay Z kutokana na zawadi hiyo huku likiwa na ushahidi baada ya mchezaji huyo kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa twitter akiishukuru Roc Nation kwa zawadi hiyo, kuweka picha na kuandika thamani yake.
“Thanks to the ROC NATION my birthday gift.” Alitweet mchezaji huyo, na kuongeza, “#2/100 made # Shawn Carter limited edition.”

0 maoni:

Post a Comment

Matangazo

Matangazo

Popular Posts

 

Blogger news

Blogroll

About