Pages

Thursday, November 7, 2013

Ilibidi iwe hivi ili kumuwezesha Rais JK kuingia bungeni jana

bungeniIli kumuwezesha Rais Jakaya Kikwete na wageni wengine akiwemo Makamu wa Rais DK Mohamed Bilal na Rais wa Zanzibar DK Mohamed Shein kuweza kuingia Bungeni leo, bunge limetengua kanuni ya 153 ikiwa ni moja ya Kanuni za Bunge toleo la 2003 ili viongozi hao wahudhurie Mkutano wa 13 kikao cha nane.
Mnadhimu Mkuu wa Serikali Waziri WILLIAM LUKUVI amesema kwa kutenguliwa kanuni hiyo na ile ya 31, wageni wataruhusiwa kukaa sehemu ya spika ambapo Rais JK atalihutubia bunge la kumi kwa mara ya pili.
Namkariri Spika Anne Makinda akisema ‘itakumbukwa hii ni mara ya pili kwa Rais kutuhutubia sisi na tuna utaratibu wa Mihimili kwa hiyo hoja hii naomba tutengue kifungu cha wageni wasiokua wabunge wasiingie humu ndani sasa, hawa tuwakaribishe’
Baada ya hiyo sentensi, Spika aliuliza maswali ya wanaounga mkono na wasiounga mkono ambapo japo kuna waliosema sioo, waliotoa jibu la ndio ndio walishinda kutokana na wingi wao.

credit:millard

0 maoni:

Post a Comment

Matangazo

Matangazo

Popular Posts

 

Blogger news

Blogroll

About