Pages

Monday, October 14, 2013

Picha: Meli kubwa zaidi kuwahi kufika Tanzania yatia nanga Dar es salaam kwa mara ya kwanza, inabeba makontena 4500


Meli yenye urefu wa mita 250 na upana wa mita 38, yenye jina la Maesk Line imetia nanga katika bandari ya Dar es salaam kwa mara ya kwanza huku ikiripotiwa kuwa ndiyo meli kubwa zaidi kuwahi kutia nanga katika bandari hiyo.
Meli hiyo ilipokelewa na waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe, ambae amesema Meli hiyo ni mali ya Maersk Shipping Company ya Denmark, na  ina uwezo wa kubeba makontena 4500.
Mwakyembe amesema kabla meli hii haijaingia nchini, meli kubwa zaidi zilizowahi kuingia nchini zilikuwa na urefu wa mita kati ya 220 na mita 234,  na zilikuwa na uwezo wa kubeba makontena kati ya 2800 na 3000.
Kwa mujibu wa waziri huyo wa Uchukuzi hapo mwanzo meli zilizokuwa zinaruhusiwa kuingia katika bandari ya Dar es Salaam hazikutakiwa kuzidi urefu wa mita 234, lakini sasa yamefanyika marekebisho ili kuendana na mahitaji ya soko la dunia.
Kuingia kwa meli kubwa kama hii kutaongeza pato la Taifa na kuchangamsha uchumi wetu.

0 maoni:

Post a Comment

Matangazo

Matangazo

Popular Posts

 

Blogger news

Blogroll

About