Pages

Friday, October 25, 2013

MJUE MTU ALIYEMRUHUSU MREMBO WA KWENYE VIDEO YA IZO B KUSHIRIKI KWENYE VIDEO ILE


24
Post hii ni maalum kwako mtu wa nguvu ambae bongofleva ni moja kati ya lishe zako bora za burudani…. nakukutanisha na mrembo ambae alionekana kwenye video ya Izzo B – ‘Love me’ ft Barnaba na Shaa.
Jina lake ni Miriam lakini wakati mwingi anatumia Kim ambapo walianza kuwasiliana na Izzo kupitia mtandao wa Instagram na kumsikilizisha wimbo wenyewe, baada ya Kim kusikiliza wimbo na kuona una sifa zake akakubali kuifanya video na ndio ikawa mara ya kwanza kuonekana kwenye video ya bongofleva.
Yafuatayo ni maswali machache kwa Miriam kutoka millardayo.com
1.Uliomba ruhusa kwa boyfriend?
Nadhani mtu pekee anaweza kunipa ruhusa ni mimi mwenyewe na Wazazi wangu, kwenye video nilijaribu kujiheshimu na kufanya kazi yangu kama msichana wa Kiafrika mwenye tabia nzuri.
2. Ni kweli kwamba siku ya kufanya video ndio ulikua unakutana na Izzo kwa mara ya kwanza?
Yeah ilikua mara ya kwanza, nilitakiwa kuonana nae saa nne lakini ikabidi niende saa nane mchana kwa sababu nilikua muoga ndio maana ikanichukua muda kwenda.23
3. Kwa nini unaitwa Kim?
Usiichukue kama ni Kim kutokana na Kim Kardashian, Kim ni jina la Baba yangu lakini shule… chuo wamependa kuniita Kim
4. Mara ya kwanza kuiona video ya ‘Love me’ ilikuaje?
Mara ya kwanza nilikua siwezi, naogopa kama nimekosea watu watanicheka, nilimuita rafiki yangu aitazame baada ya hapo akawa anapiga kelele, nilipoiangalia niliipenda.. nyumbani waliiona baada ya wiki, wa kwanza kuiona alikua mama yangu akawa anataniatania pale, na alikua hajui kama nakwenda kufanya video.
225. Baba ameiona?
Baba yangu amekasirika, hajapenda… anachotaka nisijivunjie heshima na nisirudie kufanya video.. kwa sasa nitaweka muda wangu mwingi kwenye masomo yangu chuoni Mzumbe 88.5 Morogoro mwaka wa kwanza sheria.
6.Umepata mwaliko wowote wa kuigiza movie baada ya kuonekana kwenye video?
Ni hawa watu wanaotengeneza movie, hawafiki kumi wala watano ila kwangu mimi ni wengi, wamenitafuta na kutaka kufanya kazi na mimi ila kwa sasa nazingatia kwanza masomo yangu.
21

0 maoni:

Post a Comment

Matangazo

Matangazo

Popular Posts

 

Blogger news

Blogroll

About