Pages

Tuesday, October 22, 2013

HIVI NDIVYO NDEGE ZILIVYONUSURIKA KUGONGANA ZIKIWA ANGANI

DSC_0850Wapelelezi wa Uingereza wanafanya uchunguzi juu ya tukio la kukaribia kugongana kwa ndege mbili aina ya Jumbo Jet hivi karibuni kwenye anga ya Scotland ambapo ndege hizo aina ya Jumbo Jet 747 zilikaribia kugongana zikiwa hewani saa chache baada ya kupaa huku zikiwa zimebeba abiria zaidi ya elfu moja
Waongozaji wa ndege hizo wanasema kuwa marubani wa ndege hizo hawakufuata maelekezo sahihi ambapo rubani mmoja aliomba kupewa maelekezo na alielekezwa kwenda kuifuata ndege nyingine jambo ambalo lingesababisha ajali mbaya, marubani wote waliona ndege mbele yao.
Unaambiwa aliekuepo chumba cha kuongozea ndege alikubali ombi la mmoja wa marubani kwenye ndege lililotaka ruhusa ya kutumia njia ya juu kwenye anga na akaruhusiwa lakini kumbe aliekua kwenye hicho chumba hakujua kwamba kuna ndege nyingine ambayo ilikua inatumia hiyo njia.
Baadae ndio muongozaji kwenye hiki chumba cha kuongozea ndege alishtuka ndio mipango ya kuziondoa hizi ndege kwenye njia moja ikaanza…. ilikua hekaheka ambapo walifanikiwa kuziokoa ndege kutogongana na zikakwepana kwa umbali mdogo sana.
Mara ya mwisho kwa ndege za Marekani kuponea chupuchupu kugongana zikiwa angani kama hivi ilikua ni mwaka 1978.
DSC_0849
DSC_0851
DSC_0854
DSC_0856
DSC_0857
DSC_0858
DSC_0861
125

0 maoni:

Post a Comment

Matangazo

Matangazo

Popular Posts

 

Blogger news

Blogroll

About