Pages

Monday, October 21, 2013

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA MWIMBAJI KIDUMU KUHUSU KUVUNJIKA KWA URAFIKI WA YEYE NA JULIANA

Juliana 3Kama wimbo wa ‘Haturudi nyuma’ uligusa sehemu ya mapenzi yako kwenye muziki wa Afrika Mashariki, kuna uwezekano mkubwa pia swali kuhusu video ya hii hit likawa limejirudia sana kwako.
Ni kweli, video ya hii single haikutoka na kwa kipindi kirefu hakuna kilichosikika au kueleza ni kwa sababu gani hii video haikutoka wakati single ilivunja rekodi ya hata kuwapa wawili hawa uzito na kuongeza mashabiki hasa wanaoelewa lugha ya Kiswahili.
Sasa mwimbaji Kidumu mwenye makazi yake nchini Kenya ameongea kwa mara ya kwanza na kusema ‘sitakua nafanya kolabo na mtu kama hatujaelewana… sijawahi kujua uhasama ulitokea wapi, au sijui kama mwenzangu aliridhika na hiyo kutoa tu wimbo, siku hizi kutoa wimbo bila video ni kazi nusu na ukitaka kuua wimbo fanya bila video’
‘Imeniudhi na wale wanaelewa Kiswahili wakitaka wamwambie, imeniudhi sana.. tuliperfom pamoja ila ile ilikua ni pesa tulipewa, unajua mbele ya pesa hata kama watu hawaongei wataongea siku hiyo, kwa sababu ya hii wimbo tuliahidi mashabiki kwamba video itatoka ila kwa sababu hakuna video, sihitaji kudanganya… HATUKO SAWA, yeye aendelee vile na mimi nitaendelea hivi’ – Kidumu
Kwa kumalizia Kidumu ambae ni baba wa watoto watano amesema ‘haturudi nyuma ni wimbo ulikuja haraka, nilipofanya mapenzi ya fujo nilikua na tatizo langu kwa nyumba sasa ikaonekana kuna presha flani, naambiwa uliimbaimba vitu watu wanafikiria tumevurugana sasa please fanya wimbo mwingine kuonyesha tuko pamoja, nilipoandika wimbo Juliana akaniomba kwa simu kwamba angependa tuimbe pamoja’
Kidumumillardayo.com inaendelea kuchek na Juliana Kanyomozi wa Uganda ili kusikia kutoka kwenye upande wake..
Kuwa mwanachama wa millardayo.com kwa kujiunga na facebook.com/millardayo twitter.com/millardayo na instagram.com/millardayo na kupata nafasi ya kuzipata taarifa mbalimbali pamoja na picha za matukio ya kila aina yanayotokea Tanzania na nje ya Tanzania.


0 maoni:

Post a Comment

Matangazo

Matangazo

Popular Posts

 

Blogger news

Blogroll

About