Pages

Wednesday, October 16, 2013

Hii ndio movie ya Tanzania iliyoshinda tuzo Marekani

2Nimepata Email kutoka kwa Producer Timoth Conrad ambae ni producer/writer wa hii movie ya Mdundiko yenye vichwa kama Jengua, Tinno na Dokii akisema movie yao imeshinda tuzo kwenye Silicon Valley African Film Festival (SVAFF) huko California, Marekani.
Baada ya kuipata email, nimeingia kwenye website ya tuzo zenyewe na kukuta ni kweli na list nimeiweka hapo chini.
Kwenye hii email, Conrad kutoka Timamu Effects amesema ‘kwa sasa tunasubiri matokeo yatakayotoka nchini UK ambapo pia MDUNDIKO inashindanishwa tarehe 16 Novemba 2013 ikiwania FILAMU BORA YA ASILI.
1
Timoth 1Timoth ni miongoni mwa Watanzania wachache sana ambao walipata mafunzo ya kutengeneza filamu kutoka kwa wale raia wa Marekani ambao waliwahi kutengeneza filamu kubwa sana zilizochukua headlines Afrika kama Yellow Card na nyingine ambapo mafunzo aliyoyapata yalikua ya mwezi mmoja na wiki mbili.
Ukitaka kujua utofauti wake mkubwa na maproducer wengine Tanzania tazama hiyo trailer ya movie ya Mdundiko hapo chini, movie inatarajiwa kutoka wiki chache kutoka sasa.
Hii hapa chini ndio list ya movie nyingine zilizoshinda pamoja na nchi zinakotoka..

0 maoni:

Post a Comment

Matangazo

Matangazo

Popular Posts

 

Blogger news

Blogroll

About