Pages

Monday, October 21, 2013

HAYA NDIO MAZITO ALIYOYAFICHUA JAKATE

Na Waandishi Wetu

KUMEKUWA na maneno mengi juu ya uhusiano wa kimapenzi kati ya staa mwenye vyeo vingi Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kisha staa wa kikapu wa NBA ya Marekani, Mtanzania Hasheem Thabeet Manka.


Kwa mara ya kwanza mwanadada huyo amefunguka kupitia mahojiano maalum (exclusive interview) na gazeti bora la burudani Bongo, Ijumaa Wikienda na kufichua mazito nyuma ya pazia.


Jokate ni Miss Tanzania namba 2, 2006/07. Ana kofia nyingi kama mtangazaji wa Channel O, mwigizaji, mwanamitindo, MC, mwanamuziki na video queen wa nyimbo za Bongo Fleva.

DAKIKA 150
Katika mahojiano hayo ya dakika 150 (saa 2 na nusu) yaliyofanyika katika Makao Makuu ya Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita, pamoja na uhusiano wake na mastaa hao, Jokate anayependa kucheka na kuachia tabasamu pana, alifunguka mambo mengine mengi;

Ijumaa Wikienda: Jokate kuna taarifa kuwa uliwahi kuwa na uhusiano na Hasheem Thabeet. Je, ni kweli?
Jokate: Ni kweli. Nakumbuka ilikuwa baada ya Miss Tanzania 2006. Ilikuwa kitu kama 2007 au 2008.
Ijumaa Wikienda: Uhusiano wenu ulidumu kwa muda gani?
Jokate: Miaka miwili…mitatu (kicheko).

Ijumaa Wikienda: Ulikutana wapi na Hasheem na ilikuwaje?

Jokate: Tulikutana kwenye maonesho ya mavazi kwenye Ukumbi wa Water Front, Stesheni jijini Dar. Mwanzoni tulisalimiana lakini hakukuwa na chochote kwani nilikuwa nikikutana naye nacheka vile alivyo tall (mrefu). Naye alicheka tu.

PENZI LA HASHEEM
Ijumaa Wikienda: Ilikuwaje hadi mkaingia kwenye mapenzi?
Jokate: Baada ya kuwa washkaji tukiendelea kuchati, tulijikuta tumependana sana. Mimi nilijikuta nikimpenda sana Hasheem na bado nampenda sana lakini kuna mambomambo tu yalitokea kila mtu akawa kivyake.
Ijumaa Wikienda: Maisha yako ya kimapenzi na Hasheem yalikuwaje?

Jokate: Aisee usipime…nakumbuka tulikuwa tunanunua matunda tunakaa kwenye gari tunakula. Tunatoka wote sehemu mbalimbali japo hakupenda kujianika.
Ijumaa Wikienda: Una kumbukumbu yoyote mbaya kwa Hasheem?
Jokate: Wala…japokuwa kuwa watu walikuwa wananiona nimeharibika. Labda namfuata Hasheem kwa sababu ya fedha au vyovyote walivyosema lakini mimi nilimpenda sana.

Ijumaa Wikienda: Kabla ya Hasheem kulikuwa na mwanaume mwingine?
Jokate: Yaah…lakini sipendi kabisa kumzungumzia. Namchukulia Hasheem kama mwanaume wangu wa kwanza.

‘USICHANA’
Ijumaa Wikienda: Unaposema hivyo ina maana Hasheem ndiyo alikutoa ‘usichana’.
Jokate: Nisingependa kujibu hilo lakini hadi natoka kwenye Shindano la Miss Tanzania 2006, nilikuwa sijamjua mwanaume. Nafikiri nikisema hivyo inaeleweka.

KWA NINI ALIACHANA NA HASHEEM?
Ijumaa Wikienda: Umesema ulimpenda sana Hasheem. Je, kwa nini mliachana, kumwagana au kupeana likizo?
Jokate: Ilitokea tu halafu akatokea mwanaume aliyenikuta kwenye msongo wa mawazo akawa ananiliwaza nikaona yees…nijipoze moyo.

Ijumaa Wikienda: Kabla ya kuachana mliwahi kugombana?

Jokate: Kugombana ni sehemu ya mapenzi. Ni kuonesha kuwa mnapendana. Ilitokea hivyo kwangu kwa sababu Hasheem alikuwa na heshima tofauti na wanaume wengine. Nahisi hakuna kama yeye, alinionesha alikuwa ananijali kwa kiasi gani.
DIAMOND ALIMTIBULIA
Ijumaa Wikienda: Inasemekana mwanaume huyo ni Diamond.
Jokate: Yap…ni yeye lakini kulikuwa na vitu vingi akatumia nafasi au fursa kama wanavyosema siku hizi.

ANGEMTONGOZA MWAKA HUU ANGEKULA ZA USO
Ijumaa Wikienda: Ilikuwaje?
Jokate: Sijui…ilitokea tu. Nilikuwa kwenye hali fulani akatumia nafasi hiyo lakini angenitongoza mwaka huu nisingemkubali.
Ijumaa Wikienda: Jokate haukuwa mtu aliyetegemewa kugombea mwanaume na Wema Sepetu. Huoni kuwa uliharibu mtazamo wa watu juu yako?

Jokate: Kama nilivyosema sijui nini kilitokea.
Ijumaa Wikienda: Kwani ulikutana wapi na Diamond?
Jokate: Nakumbuka nilimwalika kwenye maonesho ya mavazi yangu. Watu wengi walikuwa wakisema kuwa nimemtoa uswahilini hadi ushuani. Sikupendezwa na watu walivyokuwa wanaponda.


Naye ni binadamu, anahitaji kila kitu anachohitaji binadamu mwingine. Ukweli ni kwamba yaliibuka maneno mengi mno. Baada ya hapo kweli alikuwa ananijali sana.


HAMKOSI MWANAMKE
Unajua jamaa anajua kuimbisha na ndiyo maana anawapata wanawake wengi. Mara ananiletea chakula, zawadi, nikitaka kwenda sehemu ananipeleka. Alikuwa anataka kwenda na mimi kila sehemu.
Ijumaa Wikienda: Vipi kuhusu kufumaniwa na Wema ukiwa na Diamond hotelini?

Jokate: Nakumbuka siku moja nilikutana na Diamond hotelini kuzungumzia kazi kabla sijaingia kwenye uhusiano naye, mara Wema akatokea, alipotuona akaondoka zake. Sasa sikujua nini kinaendelea. Huku na huku nikasikia eti Wema kanifumania jamani…hahahaa…
Ijumaa Wikienda: Ulidumu na Diamond kwa muda gani?
Jokate: Kama miezi miwili hivi...


Ijumaa Wikienda: Wakati unaingia kwenye mapenzi na Diamond hukujua kama yupo na Wema?


Jokate: (akiweka uso wa kazi) Nimesema sijui nini kilichotokea na nilikuja kujikuta najuta kuwa na Diamond japo naye ni binadamu.
Ijumaa Wikienda: Uhusiano wako na Wema ukoje?
Jokate: Simchukii Wema. Sina tatizo naye. Unajua lilipotokea lile tatizo la yeye kunikashifu niliona nikiendeleza malumbano haitakuwa busara.

Ijumaa Wikienda: Kwa nini uliachana na Diamond?
Jokate: Unajua Diamond ni mtu wa kujitangaza kuwa sasa nipo na huyu na mimi sipo hivyo so hata hapo sijui nini kilitokea lakini nitafanya naye kazi. Kuna wakati nilimwambia aniandikie wimbo ‘so’ tupo kikazi zaidi.
Ijumaa Wikienda: Unajuta kuwa na Diamond?
Jokate: Najuta. Ndicho kipindi ambacho kuliibuka mambo mengi sana.

SIRI YA DIAMOND KWA WANAWAKE
Ijumaa Wikienda: Diamond ni mwanaume wa aina gani?
Jokate: Mcheshi sana. Anajua kujali. Anajua kuzungumza na mwanamke kwa maneno matamu ndiyo maana akimtokea mwanamke hamkosi.

Ijumaa Wikienda: Diamond na Hasheem nani akikurudia unakubali?

Jokate: Hakuna lakini ukweli nilimpenda sana Hasheem.

ZAWADI
Ijumaa Wikienda: Kati ya Diamond na Hasheem nani zaidi kwa zawadi?
Jokate: Naona sasa unataka kumkasirisha Diamond!
Ijumaa Wikienda: Tangu ulipoachana na Diamond una zaidi ya mwaka. Je, huna mpenzi mwingine?

Jokate: Nipo singo au unanishauri nani ananifaa?
Ijumaa Wikienda: Siwezi kuingia kwenye moyo wako wakati umesisitiza kuwa unampenda Hasheem!
Jokate: Yap…nilimpenda na ninampenda sana.

MWANA-FA VIPI?
Ijumaa Wikienda: Mbali na Hasheem, Diamond na huyo jamaa wa zamani, vipi kuhusu habari za wewe kutoka na mwanamuziki Hamis Mwinjuma ‘Mwana-FA’?


Jokate: Afadhali mnisaidie kwa sababu sijui hicho kitu kilianzia wapi. Ni uzushi tu uliosambazwa na mtu mmoja.

0 maoni:

Post a Comment

Matangazo

Matangazo

Popular Posts

 

Blogger news

Blogroll

About