Pages

Tuesday, October 1, 2013

ESTHER BULAYA ACHEMKA KWENYE INTERVIEW EATV CHANNEL 5

Mbunge wa viti maalum kupitia kundi la vijana toka chama cha mapinduzi akiwakilisha mkoa wa Mara wilaya ya Bunda alikuwa akifanyiwa mahojiano katika kipindi cha ''hot mix'' kinachorushwa kupitia kituo cha television cha EATV - Chanel 5!

Akaulizwa swali kuwa nje ya siasa anapenda kufanya shughuli gani?mojawapo ya shughuli aliyoitaja kwamba huifanya ni pamoja na kusoma vitabu na kusikiliza hotuba za wanaharakati kama Martin Luther King Jr., Mwalimu Nyerere na Mandela! 
Katika kukoleza maelezo yake akasema anapenda sana kusoma kitabu kinachoitwa ''How to be a Good Political Leader''. Mtangazaji akamuuliza jina la Author wa hicho kitabu lakini mheshimiwa mbunge akashindwa kumtaja kwakuwa alikuwa hamkumbuki pamoja na kuomba apewe muda ili amkumbuke!!

MY TAKE:
Kwa mtazamo wangu si rahisi mtu kusahau jina la author wa kitabu unachokipenda kukisoma mara kwa mara! Pengine Mh.Esther alikuwa anatafuta mileage kwamba ni msomaji mzuri wa vitabu lakini kachemka kwa kutomjua author wa kitabu akipendacho!
-JF

0 maoni:

Post a Comment

Matangazo

Matangazo

Popular Posts

 

Blogger news

Blogroll

About