Pages

Thursday, October 24, 2013

CRISTIANO RONALDO AMUONDOA RUUD VAN NISTELROOY KATIKA 3 BORA YA WAFUNGAJI BORA WA MUDA WA CHAMPIONS LEAGUE

Cristiano Ronaldo amemuondoa Ruud van Nistelrooy katika tatu bora ya ufungaji bora wa muda wote wa ligi ya mabingwa wa ulaya baada ya jana kufunga mabao mawili katika mchezo wa makundi dhidi ya Juventus. 

CHAMPIONS LEAGUE TOP 10 GOALSCORERS
NO. PLAYERGOALS
  1Raul (juu)71
  2Lionel Messi
63
  3Cristiano Ronaldo 57
  4Ruud Van Nistelrooy
56
  5Thierry Henry50
  6Andriy Shevchenko48
  7Filippo Inzaghi46
  8Alessandro Del Piero42
  9Didier Drogba41
=10Karim Benzema33
=10Fernando Morientes33
=10Zlatan Ibrahimovic33

Mshambuliaji huyo wa Los Blancos amekuwa kwenye fomu nzuri msimu katika michuano hii akifunga mabao 7 katika mechi 3 alizocheza. Kwa maana hiyo Cristiano amefikisha jumla ya mabao 57 katika mechi 95 alizocheza katika ligi ya mabingwa wa ulaya.


Cristiano Ronado ambaye sasa ndio mchezaji anayeongoza kwa kufunga mabao mengi katika michuano ya Champions League msimu huu, yupo nyuma kwa mabao 6 kumfikia Lionel Messi anayeshika nafasi ya pili na mabao 14 kumfikia Raul Gonzalez Blanco mwenye mabao 71.

0 maoni:

Post a Comment

Matangazo

Matangazo

Popular Posts

 

Blogger news

Blogroll

About