Pages

Wednesday, October 30, 2013

Alichosema David Beckham kuhusu kumkosoa Sir Alex Ferguson juu ya ile kauli

David Beckham on fergieTunafahamu kwamba siku Sir Alex Ferguson anazindua kitabu chake ambacho ameandika mambo mbalimbali kuhusu kazi yake kwa miaka yote akiifundisha club ya Manchester United, aliweka wazi kwamba alimuuza Beckham kwenda Real Madrid 2003 kwa sababu staa huyu wa soka alijiona yeye ni mkubwa kuliko Manager, alijiona mkubwa kuliko club na kwamba alipoanza mapenzi na Victoria ndio kama alianza kulegeza uzi kwenye kazi.
Pamoja na hayo maneno ambayo ndio yalipewa headlines za kutosha huku wengi wakiamini kwamba yatamkasirisha Beckham, staa huyu ameileta hii ishu kwenye upande mwingine baada ya kusema hawezi kumponda Sir Ferguson wala kusema chochote kibaya kuhusu Mwanaume huyu aliesababisha ndoto zake za kuwa staa wa soka kutimia.
Alex-Ferguson-and-David-BeckhamBeckham ambae amepongezwa na wengi kwa hekima hii, anakwambia ‘Sir Ferguson ndio aliniamini na kunipa nafasi, siwezi kukaa hapa kuongea mabaya au kumkosoa mtu alienifanya niishi kwenye ndoto yangu niliyoitaka toka kitambo’

0 maoni:

Post a Comment

Matangazo

Matangazo

Popular Posts

 

Blogger news

Blogroll

About