Pages

Friday, October 25, 2013

AIBU:CHANGU DOA AMUUMBUA MUME WA TU BAADA YA KUFANYA NGONO KWENYE GARIStori: Musa Mateja


OKTOBA 19, 2013 ilikuwa  ya aibu kwa mmiliki wa gari aina ya Toyoya Noah kufuatia kuangushiwa varangati na kahaba ambaye jina lake halikupatikana mara moja baada ya mmiliki huyo ambaye ni mume wa mtu kula naye uroda kisha kutaka kumfanyia kitu mbaya.

Tukio hilo lililojaza watu kibao, lilitokea usiku wa saa 5:19 Jumapili iliyopita ambapo kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ kikiwa katika ‘patroo’ ya kunasa matukio ya usiku.
Ilikuwa wakati OFM wakipita eneo hilo, walikuta umati ukiwa umelizunguka gari hilo huku kahaba huyo akianika ya ‘chumbani zaidi’.

Alisema: (huku ameshika jiwe) nakwambia sikubali, huwezi kunifanyia hivi. Wewe umelala na mimi kwenye gari kule halafu unakuja hapa unanitenda hivi? Jaribu kuondoa gari uone nitakavyovunja vioo.

OFM: Kwani dada ilikuwaje?

Kahaba: (huku akilia) Huyu baba amelala na mimi kule (hakutaja jina) tena ndani ya gari lake, si angalieni muone kile kiti cha upande wa abiria kilivyolala. Tumemaliza, tumekuja wote kufika hapa akanisukumia nje, nikaangukia nje na kuumia mkono. Ndiyo nikaokota jiwe ili nivunje vioo vya gari lake.

Mume wa mtu: Sasa wewe unapiga kelele za nini? Elfu kumi yako si nimekupa? Unataka nini tena, au lengo lako kunivunjia heshima?
Kahaba: Umenipa ndiyo, nataka hela ya kwenda kujitibia huu mkono ulioniumiza, nataka matibabu tu mimi.

Kahaba huyo alionesha sehemu ya mkono inayovuja damu. Aliumia baada ya kuanguka kwa kusukumwa na mwanaume huyo. 
Mwanaume huyo alitaka kuondoka kwa kuwasha gari, lakini OFM wakamzuia wakimtaka asubiri polisi kwa vile msichana huyo aliumia kiganja cha mkono wa kushoto.

Mume wa mtu: (huku akimnong’oneza sikioni OFM) jamani sikieni, tumalizane kiume. Unajua mimi nina mke na watoto, sasa kusubiri polisi hamuoni kama nitaumbuka mwenzenu?

OFM: Hamna, haatungumzii biashara yenu mliioifanya ndani ya gari, hapa tunasimamua majeraha ya mkono uliyomsababishia. 

Mashuhuda mbalimbali nao waliunga mkono OFM kwamba, mwanaume huyo asiondoke mpaka polisi wafike kushughulikia tatizo lao.


Ndipo mwanaume huyo bila kujua anaoongea nao ni OFM, alisema:

“Sawa, tusubiri polisi lakini no media (akimaanisha amekubali kusubiri polisi lakini kusiwepo wanahabari).
OFM: Ndiyo, no media, lakini polisi wanakuja sasa hivi.
Ndani ya dakika saba, mwanaume huyo alishangaa akipigwa picha na paparazi mmoja wa OFM aliyeliwahi tukio akitokea Sinza-Makaburini, Dar alikokuwa akifanya kazi nyingine za OFM.

Alipoona mwanga wa kamera ukimmulika mara kadhaa, mwanaume huyo aliingia ndani ya gari na kuondoka kwa kasi huku wananchi wakimzomea.

Cha ajabu, kahaba huyo naye alipoona mwanga wa kamera alianza kuondoka huku akisema haogopi kupigwa picha. 

Credits:Global Publisher

0 maoni:

Post a Comment

Matangazo

Matangazo

Popular Posts

 

Blogger news

Blogroll

About