Pages

Monday, September 23, 2013

JESHI la Kenya laamua kulipua sehemu ya jengo lililotekwa ili kuwakabili WAASI wa AL SHABAAB

BBC  wamearifu  kuwa vikosi vya usalama vimezingira jengo  lililotekwa na  waasi  nchini  Kenya  na hata kudhibiti sehemu ya jengo zima.

ZIFUATAZO  NI  LIVE  UPDATES:

------------------------------------------------------------------------
14:03 Mkuu wa polisi David Kimaiyo asema kuwa vikosi vya usalama vinakaribia kudhibiti hali na vimeingia ndani kabisa ya jengo hilo kiasi cha kuwaokoa baadhi ya mateka

------------------------------------------------------------------------

14:00 PM: Milipuko zaidi yasikika katika jengo hilo

13:54: Mwandishi wa BBC Idriss Situma aliye katika eneo la Westgate anasema duru zinaarifu kuwavikosi vya usalama vya Kenya vinasema kuwa ndivyo vimelipua sehemu ya jengo kujaribu kuingia ndani kabisa ya jengo hilo.

------------------------------------------------------------------------
13:52 PM Magari ya Ambulance yaobnekana yakienda katika eneo la shambulizi pamoja na magari ya zima moto. Vikosi vya usalama vinawataka watu kuondoka karibu na eneo la operesheni hiyo ili kuwawezesha kufanya kazi yao
------------------------------------------------------------------------
13:49 pm: Moshi mkubwa mweusi waonekana ukitoka juu ka juu katika jengo hilo haijulikani nini kilichosababisha
------------------------------------------------------------------------
13:19 pm Moshi mkubwa unaonekana ukitoka katika jengo la Westgate ambako wapiganaji wa Al Shabaab wanawazuilia mateka wakenya ambao idadi yao haijulikani

13:12 PM Viongozi wa kidini watoa taarifa kulaana kitendo cha Al Shabaab

12:30 PM: Milipuko zaidi na milio ya risasi imesikika katika jengo la Westgate huku vikosi vya usalama vikifanya jitahada za mwisho

0 maoni:

Post a Comment

Matangazo

Matangazo

Popular Posts

Blogger news

Blogroll

About