Pages

Monday, September 23, 2013

AGUERO, TOURE, NASRI WAPELEKA KILIO MAN UTD

Mfungaji wa mabao mawili mechi ya jana Sergio Aguero akishangilia moja ya mabao yake.
Yaya Toure baada ya kuifungia Man City bao la pili katika dakika ya 45.
Majanga: Wachezaji wa Manchester United wakiwa hawaamini kilichotokea.
Samir Nasri baada ya kuhitimisha kwa bao la nne.
Wachezaji wa Manchester City Sergio Aguero, Yaya Toure na Samir Nasri leo wamepeleka majonzi kwa Manchester United.  Wachezaji hao wameifungia Manchester City wakati ikiibuka kidedea kwa mabo 4-1 dhidi ya Manchester United kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England uliopigwa Uwanja wa  Etihad, jijini Manchester.
Sergio Aguero ameifungia Man City dakika ya 16 na 47, Yaya Toure akifunga dakika ya 45 kabla ya Samir Nasri kuhitimisha kwa bao la dakika ya 50. Manchester United wamepata bao lao la kufutia machozi dakika ya 87 kupitia kwa Wyne Rooney.
Vikosi vilikuwa hivi:
Manchester City: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Kolarov, Jesus Navas (Milner 71), Toure, Fernandinho, Nasri, Aguero (Javi Garcia 86), Negredo (Dzeko 75).
Waliokuwa benchi: Richards, Lescott, Pantilimon, Jovetic.
Manchester United: De Gea, Smalling, Ferdinand, Vidic, Evra, Carrick, Fellaini, Valencia, Rooney, Young (Cleverley 51), Welbeck.
Waliokuwa benchi: Evans, Hernandez, Nani, Kagawa, Buttner, Amos.

Global Publishers

0 maoni:

Post a Comment

Matangazo

Matangazo

Popular Posts

 

Blogger news

Blogroll

About